Johansen Buberwa – Kagera.
Mkuu wa Mkoa Kagera, Fatma Mwassa amezitaka Halmashauri zote nane za Mkoa huo kwa kipindi miezi miwili iliyobaki katika robo ya nne ya mwaka fedha 2023/2024 ziongeze kasi ya kuhakikisha inasimamia miradi ya maendeleo ili ikamilike kwa wakati.
Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa ALAT Mkoa wa Kagera kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Fatma Mwasa, Katibu Tawala Mkoa Kagera, Stephen Ndaki amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Mkoa ilikadiria kutumia bilioni 109 kwenye miradi nq imepokelewa bilioni 75 sawa na asilimia 66 na mpaka sasa imetumika bilioni 56 sawa na asilimia 73.6.
Amessma, mpaka sasa bado asilimia 26.7 ya fedha ambayo imetolewa na Serikali inahitajika ili kukamilisha miradi kwenye Mkoa huo na jukumu kubwa kwa Viongozi hao ni kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ALAT Mkoa Kagera, Wales Mashanda wakati akizungumza kwenye kikao hicho amesema fedha nyingi zilizotolewa na Serikali za ujenzi wa miradi mbalimbali itasaidia kuleta tija kwa wananchi ndani ya Mkoa huo kwenye sekta za elimu, Afya, Maji, Barabara, Umeme pamoja na utawala.
Aidha, ametumia fursa hiyo kuwaomba Viongozi kwenda kusikiliza na kutatua kero za Wananchi kwenye maeneo yao na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Baadhi ya wenyeviti wa Halmashari za wilaya Missenyi Projestus Tegamaisho na Muleba Magongo Justus wakizungumza na Dar 24 Media wamesema wanandelea kusimamia miradi vizuri ya kimkakati iliyoletwa na Serikali kwenye maeneo yao.
Aidha, wamesema pia wanasimamia miradi ya huduma za jamii kwa ubora ili kuhakikisha itakuwa na tija kwa Wananchi katika kipindi hiki cha kumaliza robo ya nne mwisho wa mwaka wa fedha 2023/2024.