Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema Wizara yake ilielekeza nguvu katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa za mafuta ya petroli, kutokana na umuhimu wake katika ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii, pamoja na kuimarisha ufanisi katika kushughulikia bidhaa hizo.
Dkt. Biteko ameyasema hayo hii leo Aprili 24, 2024 Bungeni jijini Dodoma, wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kuongeza kuwa hali hiyo ililenga kuboresha utoaji wa huduma bora kwa mujibu wa matarajio ya wadau, kuimarisha mapato pamoja na tija na ufanisi katika uendeshaji.
Amesema, “Wizara (Wizara ya Nishati) Aidha, Wizara iliendelea kuimarisha Taasisi na Mashirika yaliyo chini ya Wizara ambayo ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), pamoja na Kampuni Tanzu.
“Yatoe huduma bora kwa mujibu wa matarajio ya wadau, kuimarisha mapato pamoja na tija na ufanisi katika uendeshaji.Kwa kuzingatia gharama katika utekelezaji wa miradi ya nishati, Wizara iliendelea pia kuelekeza nguvu katika kuimarisha ushiriki wa Sekta Binafsi katika utekelezaji wa miradi ya nishati,” alibainisha Dkt. Biteko.