Serikali Nchini, imesema itaendelea na utekelezaji wa mradi wa kusambaza majiko banifu kwenye kaya zilizopo katika maeneo ya Vijijini na Vijiji-miji na kutoa ruzuku kwa wazalishaji wa mkaa mbadala kwa ajili ya ununuzi wa mashine zitakazotumika katika uzalishaji wa mkao huo.

Hayo yamesemwa leo Aprili 24,2024 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko bungeni jijini Dodoma wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.

Amesema, “tutaendelea kushirikiana na Jeshi la Magereza katika ujenzi wa Miundombinu ya nishati ya kupikia katika maeneo 211 pamoja na kuendelea na usambazaji wa gesi asilia majumbani hususani katika mikoa ya Dar es salaam, Mtwara, Lindi na Pwani.”

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema miradi ya usafirishaji wa umeme itakayotekelezwa ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Kinyerezi – Mkuranga; ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Segera na msongo wa Kilovoti 220 Segera – Tanga.

Tanzania kuwa na uhakika upatikanaji wa Petroli
Katavi: Imani za kidini zasababisha mwili kufukuliwa uzikwe upya