Baadhi ya wakazi wa Jiji la Arusha wanaofanya Biashara katika Soko kuu licha ya kupongeza Juhudi za Serikali na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa kuimarisha ulinzi na Usalama wameiomba serikali na Jeshi la Polisi kuendelea kufunga Kamera za Ulinzi sokoni hapo, ili kuendelea kidhibiti uhalifu.
Hayo wameyasema hii leo Aprili 26, 2024 wakati wa Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo Wafanya Biashara hao wamesema miaka Sitini ya Muungano imekuwa ya manufaa kwao katika biashara ambapo wamebainisha kuwa masoko ya kibiashara yamefunguka huku wakiomba serikali kuongeza Juhudi zaidi kuweka mazingira bora zaidi kwa wafanyabiashara hao.
Aidha wafanya biashara hao wamesema kuwa wamepokea kwa mikono miliwi tamko la Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Paul Makonda alilolitoa hivi karibuni ambapo alitoa ahadi yake ya kuweka utaratibu wa Jiji hilo kufanya Biashara Masaa ishirini nne ili kukuza uchumi wa Mkoa huo.
Walisisitiza kuwa mpango wa Jeshi la Polisi wa kufunga kamera za ulinzi katika jiji hilo limekuja na matokeo chanya ambapo wamebainisha kuwa uhalifu umepungua kwa kiasi kikubwa huku wakiomba serikali na Jeshi hilo kufunga kamera za kutosha katika Soko Kuu la Jiji la Arusha.