Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezungumza mbele ya Viongozi wakuu wa Afrika na kusema, “ushirikiano wa IDA umesaidia kuboresha viashiria vya afya ya uzazi na mtoto pamoja na viwango vya upatikanaji wa umeme vijijini, upatikanaji wa maji salama ya kunywa pamoja na kufufua uchumi kwa upana zaidi.”
Rais Samia aliyasema hayo katika mkutani huo uliofanyika nchini Kenya na kuongeza kuwa “kwa kupitia IDA, tunaamini inastahili kuangazia juhudi za pamoja za mafanikio.”
Aidha, Rais Samia aliongeza kuwa, “tuna mradi wa maendeleo wa Bonde la Mto Msimbazi kutoka Benki ya Dunia wenye gharama ya Dola Milioni mbili, ambao utasaidia kupunguza athari za mafuriko na uboreshaji mipango miji.”