Wafanyabiashara wa Soko la Mawenzi Mkoani Morogoro, wamelalamikia adha wanayoipata kutokana na kufumuka mara kwa mara miundombinu inayopitisha maji taka katika eneo hilo na kusambaa katika maeneo yao ya kazi kitu ambacho ni hatari kwa afya ya binadamu.

Wakizungumza na Dar24 Media Wafanyabiashara hao wamesema wanaiomba Mamlaka husika kufanya matengezo kwenye chemba hizo kwani mbali na uwezekano wa kudhuru afya za binadamu pia zinachafua mazingira.

Akijibu hoja hiyo Mkurugenzi wa Idara Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira, Mhandisi Thomas Mbulika amewataka Wananchi kuacha tabia ya utupaji taka ngumu kwenye vyoo, kwani ndio sababu kuu ya miundombinu hiyo kuziba na kufumuka mara kwa mara na kudai kuwa tayari wameshafika eneo la tukio na matengezo yanaendelea.

Hata hivyo, ikumbuke kuwa usambaaji wa maji taka unachangia kwa asilimia kubwa kuibua magonjwa kama vile kipindupindu, hivyo upo umuhimu wa kutunza mazingira kwa manufaa ya afya ya jamii.

RC Sendiga: RUWASA endeleeni kutoa huduma bora kwa Wananchi
Simba Queens yasaka rekodi Ligi Kuu