Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Daniel Sillo amewapongeza waandishi wa habari wa mkoa wa Manyara kwa kuanzisha mfuko wa pamoja wa kusaidiana.
Sillo ambaye ni mbunge wa Jimbo la Babati vijijini ametoa pongezi hizo mara baada ya kukutana na wanachama wa mfuko huo mjini Babati kwa lengo la kushauriana nao kuhusu namna ya kuboresha mfuko ambapo amehidi kuwachangia ili wafikie malengo yao.
“Mifuko ya namna hii ni muhimu sana kwa watu mnaofanya kazi za kitaalamu zinazofanana kama nyie ndugu zangu wana habari. Japo mmechelewa lakini niwapongeze mmeanza maana hata sisi wabunge tunao mfuko kama huu wa kufarijiana”. Amesema Sillo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa mfuko huo Joseph Burra amesema lengo ni kusaidiana wenyewe kwa wenyewe wakati wa kuuguliwa, kufiwa na pia kuwezeshana kwa njia ya mikopo ili kujikwamua kiuchumi.