Idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko katika fampo la taka jijini Kampala imefikia watu 25, huku matumaini ya kuwapata manusura zaidi yakiendelea kufifia.

Tukio hilo, lilitokea Agosti 10, 2024 katika Wilaya ya Kiteezi iliyopo Kaskazini mwa jiji kuu la Kampala, baada ya kuanza kwa maporomoko ya ardhi yaliyosabajishwa na Mvua katika eneo la kutupia taka.

Waziri wa majanga nchini Uganda, Lillian Aber amesema hadi kufikia Jumatatu jioni (Agosti 12, 2024), miili 25 ilikuwa imepatikana na hakukuwa na manusura.

Hata hivyo, inaarifiwa kuwa Mvua kubwa zikizonyesha zimeathiri shughuli za kupata miili zaidi, huku Rais Yoweri Museveni akiliagiza Jeshi kutoa usaidizi katika zoezi hilo.

Watano mbaroni kwa wizi wa Injini 12 za Boti
Chato: Katimba awataka CHMT kujitathmini