Takribani Watu saba wakiwemo watoto wanne wamefariki huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC, baada ya watu wenye silaha kushambulia lori la mafuta huku bomu lililokuwa likichezewa na Watoto likilipuka.

Kiongozi wa kikundi cha Vijiji vilivyopo eneo la Rutshuru, Jerome Nyamuhanzi amesema Lori hilo liliwaka moto baada ya shambulio karibu na mji wa Katwiguru katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Amesema, “baada ya shambulio hilo, bomu lililokuwa limetegwa lilichukuliwa na watoto, ambao walidhani ni kitu cha kuchezea hivyo kililipuka na watoto wanne walikufa papo hapo.”

Katika tukio hilo, Watu sita walijeruhiwa ambao nao walisemaa mlipuko hio ulisababisha vifo vya watu wasiopungua saba wakiwemo watoto hao.

Maisha: Hii hapa dawa ya matapeli wa Viwanja
Tetesi za usajili Duniani leo Agosti 16