Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, CPA. Shaaban Mpendu amewapongeza wananchi wa Jimbo la Babati Mjini kwa kuendelea kujitokeza Kwenye Kujiandikisha na Kuboresha taarifa katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura katika Vituo vilivyopo kwenye makazi yao Mkoani Manyara.

CPA Mpendu amewataka Wananchi ambao bado hawajajitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa katika Daftari la Wapiga Kura wafanye hivyo ili waweze kupata nafasi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka katika Uchaguzi wa 2025.

Aidha, CPA Shaaban ameboresha taarifa zake katika moja ya Kituo kilichopo Jimbo la Babati Mjini na kupatiwa kadi ambayo inampa nafasi ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 katika JImbo hilo.

Nao Mawakala waliopo katika Vituo vya Kujiandikisha wamesema kuwa mwitikio ni mkubwa na wamewahimiza Vijana kuendelea kujitokeza kwa wingi zaidi katika Kujiandikisha na kuboresha taarifa katika Daftrai la Kudumu la Wapiga Kura.

Bashungwa awasilisha mkakati kuwawezesha Wakandarasi wazawa
Chalinze wapewa siku sita kumaliza kero ya Maji