Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kufanya Sensa ya Uzalishaji viwandani kwa kuanzia mwezi machi hadi Juni 2025.
Akizungumza na Waandishi wa habari Waziri wa Viwanda na Biashara Seleman Jafo leo Febuari 5 Jijini Dodoma, ambapo amesema, Sensa ya viwanda mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2013.
“Kwa mujibu wa Sensa hiyo Tanzania ilikuwa na jumla ya viwanda 49,243 ambavyo vilikuwa vimegawanyika katika makundi makuu manne kulingana na Sera ya Viwanda vidogo na biashara ndogo,” amesema.
“Viwanda vidogo sana vilikuwa 41,919, viwanda vidogo 6,907, viwanda vya Kati 170 na viwanda Vikubwa 247,” amesema Jafo.
Hata hivyo, 0amesema taarifa za viwanda zitakazo kusanywa zitahusisha shughuli za kiuchumi zilizofanyika katika viwanda.
“Shughuli hizo zitajumuisha utengenezaji wa bidhaa viwandani,uchimbaji wa madini na kokoto,uzalishaji na usambazaji wa umeme,gesi mvuke na kubadilisha hali (Joto,baridi) na usambazaji wa maji safi, mifumo ya kukusanya maji taka, udhibiti wa taka na shughuli za urejeshaji”
Amesema Sensa ya Uzalishaji viwandani itakusanya taarifa kutoka viwanda vyote ambavyo vimegawanyika katika makundi mawili.
“Kundo la Viwanda vyenye wafanyakazi kuanzia kumi au zaidi, na kundi la viwanda vyenye wafanyakazi kuanzia mmoja hadi tisa”, amesema
“Aidha kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi kwa viwanda vidogo zitafanyika kwa sampuli kutokana na wingi wa viwanda na sifa zinazofanana,” amesema Jafo