Wakala wa Barabara Nchini –  TANROADS na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini – TARURA, wametakiwa kushughulikia barabara ambazo Wananchi waliahidiwa katika kampeni za CCM za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, ili zisije kuleta msuko kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge ameyasema hayo katika mkutano wa bodi ya barabara ya mkoa iliyofanyika mjini Kibaha mkoani Pwani kwa kuhusisha wadau mbalimbali wa Maendeleo na wataalamu.

Amesema, ni lazima kuwe na mipango ya utengenezaji wa barabara kwa maendeleo katika mkoa kwa kuanzia kwanza barabara ambazo waliahidi Wananchi kwamba zipi zimekamilika na zipi bado zipo katika utekelezaji na zipo kwenye hatua gani.

“Na tuone na zile barabara ambazo hatujaanza kabisa na tujue kipaumbele ni barabara zipi na zitakamilishwa kutokana na fedha zipi na waheshimiwa Wabunge watueleze ni barabara zipi zipewe kipaumbele hata kama ni tano hata kumi zipi hizo zipewe kipaumbele zitatupa msukosuko mkubwa” alisema.

Kunenge ameongeza kuwa, “angalieni zipi mmezitekeleza na zipi bado hamjazitekeleza na tutoe sababu kwanini hatujazitekeleza na tuone kama tutaenda nazo kwani tunafahamu tuna majukumu mengi lakini hizi barabara tukiziangalia zinaweza kutupa unafuu.”

Dkt. Mfaume ataka ubora wa Miundombinu uendane naubora wa Huduma
Serikali inatambua umuhimu wa kukuza usawa wa kijinsia - Majaliwa