Mpango huo ulopewa jina la “Fufua nguvu za kijeshi za Ulaya” umeidhinishwa baada ya wiki kadhaa za mkanganyiko wa nchi za Ulaya, juu ya mahusiano kati ya kanda hiyo na mshirika wao wa jadi, Marekani.
Ulaya inahofia kitisho cha Urusi tangu utawala mpya wa Rais Donald Trump ulipoonesha dalili ya kutowatunga mkono washirika.