Jumla ya Wanajeshi 10 na watuhumiwa 19 wa uhalifu wameuawa nchini Mexico, katika operesheni ya kumkamata Ovidio Guzman ambaye ni mtoto wa kiume wa muuzaji maarufu wa dawa za kulevya Joaquin Guzman, maarufu kama El Chapo.

Waziri wa Ulinzi wa Mexico, Luis Cresencio Sandoval, amewaambia waandishi habari kuwa kutokana na tukio hilo kwa bahati mbaya wanajeshi 10 walipoteza maisha yao watimimiza majukumu yao ya kikazi.

Ovidio Guzman, mtoto wa kiume wa muuzaji maarufu wa dawa za kulevya Joaquin Guzman, maarufu kama El Chapo. Picha ya Mitu.

Sandoval amesema wahalifu 19 waliovunja sheria pia waliuawa katika operesheni hiyo iliyofanyika Januari 5, 2023 na kwamba jeshi na walinzi wa Taifa wamefanikiwa kumkamata mtoto huyo wa El Chapo, mwenye umri wa miaka 32.

Baba mzazi wa mtoto huyo (Joaquin Guzman), anatumikia kifungo cha maisha nchini Marekani kwa kusafirisha mamia ya tani za dawa za kulevya nchini humo katika kipindi cha miaka 25.

Serikali kuendeleza uboreshaji sekta ya Afya: Dugange
Wawili wafariki kwa Treni Kilimanjaro