Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema imebaini ongezeko la udanganyifu wa fedha nchini unaohusisha Wananchi kupokea taarifa ya hati au barua pepe inayodai kuwa ni uthibitisho wa malipo kupitia mifumo ya uhamishaji fedha.

Kupitia taarifa iliyotolewa hii leo Januari 6, 2023 na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya
BoT imeeleza kuwa mpokeaji hufahamishwa kuwa fedha zimeingizwa kwenye benki au akaunti katika taasisi ya fedha nchini Tanzania jambo ambalo si la kweli.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, “Mpokeaji fedha huelekezwa kulipa kiasi fulani cha fedha kuwezesha kupata fedha hizo nyingi hivyo, Benki Kuu inautaarifu umma kuwa taarifa hizo ni za kughushi na za kubuni, Wananchi wanashauriwa kuwa waangalifu na kuacha kujihusisha na miamala hiyo ambayo kwa kawaida inalenga kuwatapeli.”

Aidha, BoT pia imewataka wananchi kuzingatia kanuni bora za kufanya miamala ya fedha ili kuepuka upotevu wa fedha ambazo ni kuhakikisha usalama wa taarifa za fedha wakati wa kutoa taarifa binafsi mtandaoni (tovuti, mitandao ya kijamii), kupitia barua pepe au simu.

Ajali Tanga: Maroli yagongana Watatu wafariki
Majaliwa akubali maboresho ujenzi Hospitali Namtumbo