Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange amesema Serikali itaendelea kuiboresha sekta ya afya ikiwemo kununua magari mawili kwenye halmashauri zote 184 nchini moja likiwa la wagonjwa na lingine kwa ajili ya usimamizi wa huduma za afya.

Dkt. Dugange, ameyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, aliyoifanya Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma, ambayo aliitumia kukagua maendeleo ya utekelezaji wa agizo alilolitoa Oktoba 18, 2022 alipofanya ziara hospitalini hapo na kuridhishwa na kazi iliyofanyika.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange.

Awali akizungumza kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Namtumbo, Dkt. Dugange amesema watahakikisha wanasimamia maagizo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuu, ili kuhakikisha shule hiyo inakamilika kwa wakati na inaanza kudahili wanafunzi.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Christopher Wabarumi aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo na wilaya hiyo ambayo inaendelea na ujenzi wa majengo ya 22 katika hospitali ya wilaya hiyo.

Mawaziri wawili kuzuru nchini Ethiopia
29 wafariki tukio la kumkamata mtoto wa El Chapo