Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock, na Waziri wa Mambo ya Nje wa wa Ufaransa, Catherine Colonna, wanatarajia kuizuru nchini Ethiopia wiki ijayo.

Ofisi ya Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani, imesema mawaziri hao watafika Ethiopia ili kushuhudia mpango mpya wa amani unaoratibiwa katika jimbo lenye mzozo la Tigray.

Wananchi wa Ethiopia. Picha ya The New York Times.

Wanadiplomasia hao, pamoja na mambo mengine watafanya mazungumzo na Serikali ya Ethiopia na Umoja wa Afrika kujadili masuala ya usalama barani Afrika.

Serikali ya Ethiopia ilifikia makubaliano ya amani na wapiganaji wa Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF mwezi Novemba na ilifunga mawasiliano ya simu, benki, umeme na usafiri wa anga katika jimbo la Tigray.

Dkt. Tax awataka Watumishi kuboresha utendaji
Serikali kuendeleza uboreshaji sekta ya Afya: Dugange