Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefanya tena ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam na kukuta udanganyifu mwingine mengine.

Majaliwa alifika Bandarini hapo na kufanya ukaguzi kwenye mfumo wa kufanya ukaguzi na malipo baada ya kupata taarifa kuwa kuna makontena 2431 yaliyotolewa bandarini hapo bila kulipa kodi.

Ripoti ya ukaguzi ya kuanzia mwezi Machi hadi Septemba 2014 ilionesha kuwepo upotevu wa makontena hayo yaliyopitia katika bandari kavu (ICD) nne tofauti.

Baada ya kuipitia ripoti hiyo, Waziri Mkuu alibaini kuwa ni watumishi 10 tu tena wa ngazi za chini ambao walisimamishwa kazi huku wale wa ngazi za juu wakiachwa huru.

“Hapa naona mmewachukulia hatua watu kumi tu, tena vidagaa, wale nyangumi hawamo.” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu aliagiza kupitiwa upya kwa majina ya watu waliohusika na kupelekewa majina ya waliochukuliwa hatua na wale wote ambao hawakuchukuliwa hatua.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa alimhoji Kaimu Meneja wa Bandari hiyo, Hebel Mhanga kuhusu mfumo unaotumika kufanya malipo ya mizigo kubaini kuwa mfumo uliopo unatoa mwanya wa kutorosha mizigo bandarini hapo licha ya Kaimu Meneja huyo kujaribu kuutetea.

Alimuagiza Naibu Kaimu Meneja wa Bandari hiyo kuhakikisha anafanya mabadiliko ya mfumo huo ndani ya siku saba na kuweka mfumo wa malipo kwa njia ya kielekronini (e-payment).

“Watafuteni mafundi kwa gharama yoyote ile, wafanye kazi mfumo wa e-payment uanze kutumika baada ya siku saba,” aliagiza.

Magufuli Atoa Siku Saba Kwa Wafanyabiashara Waliokwepa Kodi
Nawapa siku 7 wakwepa kodi wote jisalimisheni - Magufuli