Mwimbaji wa Uingereza, Adele amevunja rekodi nyingine ya YouTube kwa video yake ya ‘Hello’ kuwa ya kwanza kufikisha idadi ya watazamaji bilioni 1 ndani ya kipindi cha miezi mitatu tu, tangu mtandao huo uanzishwe.

Jana, YouTube walitangaza kuwa wimbo wa Adele umefikisha idadi ya views bilioni 1 katika siku yake ya 87, hivyo kuvunja rekodi ya siku 158 iliyokuwa ikishikiliwa na video ya PSY, “Gangnam Style”.

Video ya Hello sasa inaungana na video nyingine 16 duniani zilizofikisha watazamani bilioni 1.

 

Nyimbo hizo ni pamoja na  Sugar ya Maroon 5, Lean On ya Major Lazer’, Counting Stars ya OneRepublic, Party Rock ya LMFAO na Chandelier Sia. Wengine ni Waka Waka ya Shakir, Thinking Out Loud ya Ed Sheeran na Love Me Like You Do ya Ellie Goulding.

Star wa Nigeria aendelea kusisitiza kuwa Wizkid amemuibia
Picha: Rihanna na Leonardo DiCaprio wakipigana 'Mabusu' zanaswa