Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimeeleza kushangazwa na hatua ya kuitwa kwa Watendaji Kata nchini ambao wametakiwa kufika Ikulu jijini Dar es salaam ifikapo Septemba 02, 2019.
Akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya Nje CHADEMA, John Mrema, amesema kuwa wana wasiwasi na kitendo hicho.
“Kitendo cha Serikali kuwaita watendaji wa ngazi ya chini kabisa hakijawahi kutokea kwenye nchi yetu, tulitegemea kama kuna maagizo yangeweza kutoka TAMISEMI, hadi chini, kitendo cha Serikali Kuu kuwaita watendaji maanake watendaji wa TAMISEMI wameshindwa.” amesema John Mrema
Akijibu madai hayo kwenye kipindi hicho Waziri Jafo, ameeleza kushangazwa kwa namna ya jambo hilo lilivyopokelewa katika namna ya kisiasa.
“Ni jambo la ajabu sana kama kila jambo wanataka kulipeleka kisiasa, taifa haliwezi kwenda mbele, watu tuko kazini nadhani kila kitu kikitafsiriwa kisiasa nadhani tutakuwa hatuitendei haki Tanzania yetu, watu wawaache viongozi wa Serikali wafanye kazi.” amesema waziri Jaffo
Hata hivyo, hivi karibuni kulisambaa barua ikionyesha kuitwa kwa Watendaji wa kata nchi nzima ambao watakutana na Rais Magufuli Septemba 02 mwaka huu.
-
Dkt. Bashiru ampongeza Askari aliyegoma kutumia salamu ya CCM
-
Waziri Mkuu afanya mazungumzo na viongozi wa Toshiba
-
Mama Samia akanusha taarifa za Urais