Jeshi la polisi limezuia mkutano wa mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia leo Machi 5, 2020 huku akitakiwa kuripoti katika kituo kidogo cha polisi Ruangwa.
Mkutano huo wa ndani ulikuwa unatarajiwa kufanyika baina ya wanachama wa NCCR na Mbatia leo baada ya kufika jimbo la Busokelo majira ya saa tano asubuhi katika kijiji cha Kandete.
Akizungumza nje ya ukumbi wa mkutano, Mbatia amesema kwa sasa hawezi kuzungumza lolote juu ya zuio hilo mpaka atakapofika Polisi nakujua anaitiwa nini na kuna shida gani.