Uongozi wa klabu ya Young Africans na wadhamini wa klabu hiyo kampuni ya GSM wamehaidi kutoa Shilingi milioni 200 kwa wachezaji, iwapo watashinda mchezo wa jumapili dhidi ya Wekundu Wa MSimbazi Simba utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Young Africans, Afisa muhamasishaji wa klabu hiyo kongwe nchini, Antonio Nugaz amesema wadhamini kampuni ya GSM wameweka mezani Shilingi milioni 200 kwa wachezaji, endapo watapata ushindi wa aina yoyote siku hiyo.

“Hata wakichukua ubingwa sio tatizo, tunachohitaji ni kuwachapa, nadhani raha ya ubingwa utakuwa umeisha na kuwanyamazisha kupiga kelele hovyo mtaani.

“Tulikuwa na utaratibu wa kutoa motisha kila wanaposhinda kwenye michezo ya Ligi Kuu hupewa Sh 10Milioni, lakini kutokana na umuhimu wa mchezo wa Jumapili tumeamua kufanya kitu kwa wachezaji ili kuweka raha Jangwani,’ alisema Nugaz.

Aliongeza kocha, Luc Eymael amemweleza kuwasoma Simba kwa muda mrefu tangu alipowasili nchini kukinoa kikosi hicho na amegundua mambo mengi ya kuwadhibiti wapinzani wao.

“Luc ameniambia atashambulia mwanzo mwisho kwa kasi, tofauti na michezo iliyopita kwani, Boniface Mkwasa (kocha Msaidizi wa Young Africans) amemweleza vitu vingi kuhusu mchezo huo.”

Tanzania mfano SADC mafunzo ya uzoefu wa kazi kwa vijana
Jeshi la polisi lazuia mkutano wa Mbatia Busokelo