Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema ameachiwa kwa dhamana leo Machi 5, 2020 baada ya kushikiliwa Polisi tangu Jumatatu Machi 2, 2020.

Lema alienda kuripoti Ofisi ya Mkuu wa upelelezi wa Polisi (RCO) Arusha kama alivyotakiwa kufanya baada ya kupigiwa simu na Polisi ambao walienda kwake na kumkosa.

Baada ya hapo alisafirishwa kwenda Kituo Kikuu cha Polisi Singida ambapo alihojiwa akituhumiwa kutoa taarifa za upotoshaji zenye lengo la kuchonganisha Jeshi hilo na Wananchi.

Aidha, Katibu wa CHADEMA wilaya Singida Mjini, alisema Lema alimwambia kuwa kosa analodaiwa kutenda ni kutaja orodha ya watu 14 waliouawa Manyoni kwa kuchinjwa na kuchomwa moto.

Jeshi la polisi lazuia mkutano wa Mbatia Busokelo
Tanzania haina upungufu wa ARV