Mbunge wa CCM jimbo la Muleba Kusini, Anna Tibaijuka amesema Rais John Magufuli amewapa nguvu wananchi wanaoamini katika dawa za asili ambapo amesema dawa ya asili si uchawi ni sayansi.

Tibaijuka amesema kwakutumia sayansi hiyo itasaidia sana wazee na watoto kwasababu huwa wanasumbuliwa na nimonia hivyo wanaobeza watambue kuwa hiyo ni elimu ya kawaida sio ramli.

Italia wamsaka ‘mchawi wa corona’, Merkel aionya Ujerumani

“Kwa hili namshukuru Rais Dk. John Pombe Magufuli kutambua tiba za asili kwenye vita hii ya Corona, dawa za asili si uchawi ila ni sayansi,” amesema Tibaijuka.

Ikumbukwe hivi karibuni Rais John Magufuli wakati akiongea na wakuu wa vyombo vya ulinzi kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 alisema ni wakati sahihi wa watu kuanza kutumia tiba za asili ikiwemo kujifukiza ili kupambana na ugonjwa huo.

Mawaziri G20 kusaidia soko la ajira

Wakenya waliopo China kurudishwa mei 1

Tetemeko lenye ukubwa 4.6 laikumba Kanda ya Ziwa Victoria
Kenya kufanyiwa jaribio chanjo ya Corona