Serikali nchni Uganda umewarudisha takribani madereva 14 wa maroli (8 Tanzania na 6 Kenya) baada ya kubainika kuwa wameathirika na virusi vya Corona.
Hayo yamebainishwa na wizara ya afya nchi humo licha ya kuwa bado haijafahamika endapo madereva hao wamepona au watenedelea na matibabu nchi mwao.
Wakati Serikali nchi Uganda na watu wake wakiwa wanachukua tahadhari ya kukaa ndani ili kuzuia maambukizi ya corona, maderava wa maroli ya mizigo kutoka Tanzania na Kenya wameonekana kuwa kikwazo kwa kuingia na virusi hivyo.
Hata hivyo wizara ya afya nchini humo imekuwa ikisisitiza kuwa madereva wanaoingia wanatakiwa kupimwa kwanza kwenye nchi zao kuepuka kusambaza virusi hivyo kwenye nchi hiyo yenye visa 79 hadi sasa.