Wizara ya afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza ongezeko la wagonjwa 7 wa homa kali ya mapafu covid -19 na kupelekea idadi jumla ya visa kufikia 105.

Taarifa iliyotolewa mapema leo imeeleza kuwa wagonjwa wapya wote ni raia wa Tanzania na wote wanatokea kisiwa cha Unguja.

Jumla ya wagonjwa 36 wamepona na kuruhusiwa kurudi nyumbani, wakishauriwa kubaki ndani kwa siku 14 huku wataalamu wa Afya wakiendelea kuwafuatilia.

Serikali imetoa wito kwa wananchi kuendeea kuchukua tahadhari. Pia kwa wenye dalili wametakiwa kupiga simu namba 190.

Uganda yawarudisha Madereva wenye Corona Tanzania, Kenya
Pluijm awakumbusha Young Africans misingi ya usajili