Mdogo wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anayefahamika kwa jina la Bernard Lowassa, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo, Aprili 28.

Mtoto wa Edward amethibitisha kutokea kwa kifo cha babayake mdogo alipoongea na EATV mapema leo na kusema kuwa amefariki katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Fred Lowassa amesema familia inakutana kupanga taratibu za mazishi, baba yake Edward Lowassa amepata mshtuko kidogo lakini hali yake inaendalea vizuri

Enzi za uhai wake, Bernard Lowassa alikuwa ni Mkurugenzi wa kampuni ya AGE Insurance Brokers.

Selasini kutimkia NCCR-Mageuzi
Uganda yawarudisha Madereva wenye Corona Tanzania, Kenya