Mbunge wa Rombo, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)  Joseph Selasini ametangza kujivua uwanachama wa chama hicho na kujiunga na chama cha NCCR – Mageuzi.

Akitangaza uamuzi huo leo April 28, 2020 wakati akiongea na waandishi wa habari ameeleza kitendo cha kutengwa ndani ya chama na kutolewa kwenye kundi la mtandao wa Whatsapp tangu April 25 ambapo amesema kundi hilo ni nyenzo muhimu ya kazi na uongozi shirikishi ndani ya chama hicho kimemfanya afikie uamuzi huo.

Baadhi ya mataifa kulegeza masharti ya kukabiliana na Corona

Hata hivyo Selasini amekuwa akihusishwa kukihama chama hicho tangu January 14, 2020, alipojivua nyadhifa ya Mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni kwa sababu yakutokutambulishwa rasmi kwa uongozi wa Bunge tangu ateuliwe mika miwili iliyopita.

Amesema kuwa kipindi chake cha ubunge kitakapo fika ukomo mwaka huu mwezi October ndipo atakapo achana rasmi na chama hicho.

Kim Jong-un azungumza kwa mara ya kwanza tangu azushiwe kufa

Bashungwa atangaza Ukomo bei ya barakoa 1,500/=

Rage hachoki kuwatania Young Africans
Mtoto wa Lowasa athibitisha kifo cha Bernard Lowasa