Mtendaji mkuu wa mabingwa wa kombe la shirikisho Tanzania bara (ASFC) Azam FC Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amefichua kuwa staili ya ushangiliaji ya mshambuliaji wa klabu ya Simba, Meddie Kagere imesababisha apige marufuku nyumbani kwake TV isiwashwe akiwa hayupo.
Akipiga stori katika InstaLive na mchambuzi Ally Kamwe, Popat alisema, kila alipokuwa akirudi nyumbani mtoto wake alikuwa akimpokea kwa kufunga jicho moja kama anavyofanya Kagere kila anapofunga bao.
“Mwanzo nilikuwa sielewi anamaanisha nini, lakini siku nipokuwa nyumbani tukiangalia TV, alipomuona Kagere, akanigeuka na kufunika jicho lake kwa mkono wake.”
“Kuanzia hapo nikaweka sheria, hakuna TV kuwashwa mpaka ninapokuwa nimerudi nyumbani” alisema Popat
Mjadala huu ulikuja Popat alipokuwa akielezea jinsi vyombo vya habari vinavyowapa nafasi kubwa sana Simba na Yanga hivyo watoto kushindwa kuchagua timu nyingine za kushabikia.