Mkongwe wa muziki wa dansi Tanzania, Mafumu Bilal Bombenga maarufu ‘Super Sax’, amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari muda mrefu.

Mke wa Mafumu amethibitishia kuwa mumewe amefariki, na hali yake ilibadilika jana Mei 11.

Mafumu alijifunzia kupiga Saxophone mwaka 1972 akiwa JKT Makutupora kwenye Brass Band yao, alikuwa akisumbuliwa na Kisukari kwa muda mrefu hali iliyopelekea kukatwa kwa mguu wake mmoja.

Mkongwe huyo ameimba kwenye bendi ya African Stars ambayo hata jina lake alilibuni yeye na kutamba na vibao kama Sakatu Sakatu, Mayanga, Maya, Afrika na Dance Dance.

Aidha, enzi za uhai wake alitamba pia na bendi kadhaa zikiwemo Maquis, MK Group, Bicco Stars, Bima Lee, African Stars na African Beats.

Majembe mawili anayoyakubali Ibrahim Ajibu
Kagera apeleka balaa nyumbani kwa Popat