Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa soka Tanzania bara Wekundu Wa Msimbazi Simba Ibrahim Ajibu, amesema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao alikuwa na muungano nao bora ndani ya uwanja ni pamoja na Obrey Chirwa anayekipiga ndani ya Azam FC pamoja na Erasto Nyoni.

Ajibu alicheza na Chirwa msimu wa 2017/18 ambapo alitoa jumla ya pasi nne za mabao na katika mabao hayo matatu yalifungwa na mshambuliaji huyo kutoka nchini Zambia.

Nyoni ni beki ndani ya Simba ambayo imecheza michezo 28 na kufungwa mabao 15 msimu huu wa 2019/20 ikiwa na pointi 71 kibindoni.

Ajibu amesema:”Ni wachezaji wengi ambao ninapenda kushirikiana nao kwani ninafanya nao kazi kwa ukaribu ila miongoni mwao ni Chirwa ambaye nilikuwa naye Young Africans na alifunga mabao mengi huku nami nikihusika kutengeneza pasi za mabao.”

“Kuhusu Nyoni lazima uwe na beki ambaye atakupa ulinzi na uwezo wake pia wa kufunga ni muhimu hasa timu inapotafuta ushindi.”

Benki Kuu yashusha riba za mikopo kukabiliana na Corona
Kisukari chakatisha uhai wa Mkongwe wa dansi Mafumu Bilal