Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ngazi ya Makatibu Wakuu wamekutana na kujadili rasimu ya mpango mkakati elekezi mpya wa maendeleo wa kanda (2020 – 2030) pamoja na rasimu ya dira ya SADC (2020 – 2050) kwa njia ya (Video Conference) jijini Dar es Salaam.
Akiongea mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Mwenyekiti wa mkutano ambae ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Brigedia Jenerali, Balozi Wilbert Ibuge amesema kuwa lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuangalia mambo mawili makubwa ambayo ni dhima ya SADC, kuanzia 2020 hadi 2050
“Nyaraka hizi mbili ni za muhimu sana kwa sababu hadi sasa hivi toka SADC ilipoanzishwa 1992 imefanya mambo makubwa lakini sasa ule mpango mkakati wake uliokuwa unatumika tangu mwaka 2010 na ambao ulihuishwa mwaka 2015 ukafika hadi 2020 umeisha muda wake hivyo ilikuwa ni muhimu kuandaa rasimu ya nyaraka hizi muhimu,” Amesema Balozi Ibuge.
Ameongeza kuwa, rasimu za nyaraka hizo mbili zitawasilishwa kwenye mkutano wa 40 wa Wakuu wa nchi wanachama wa SADC na Serikali unaotegemewa kufanyika tarehe 17 Mwezi Agosti 2020 kwa njia ya mtandao.
“Kumekucha” Membe achukua fomu ya Urais
“Dira ya SADC 2020 – 2050 inatoa taswira ya Jumuiya kwa miaka 30 ijayo ambapo msingi wake ni amani, ulinzi, utulivu na utawala bora, uchumi wa kati unaoendeshwa na sekta ya viwanda na wanajumuiya wenye hali bora ya maisha,” Amesema Balozi Ibuge.