Manjano ni kiungo ambacho hutumika katika mapishi, lakini wengi hutumia unga wake kupatka usoni ili kuwa na muonekano mzuri wa ngozi.
Matumizi ya viungo kwa ajiri ya afya ya urembo kwa binadamu yahitaji utafiti ili kujua ni kiwango gani unachopaswa kutumia ili kupata faida zinazohitajika kiafya.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la The Jounal ofa Nutrition and Intermediary Metabolism, umeeleza kuwa manjano pia yanaweza kusaidia kupunguza kiwango cha sukari kwa wagonjwa wa aina ya pili ya kisukari.
Inasaidia uwiano wa sukari
Manjano imesaidia kongosho katika uchujaji wa sukari kama ilivyo katika matibabu ya kisukari, pia inasaidia kongosho kumudu kiwango cha sukari mwilini ambayo inaweza kukomesha kutokea kwa kisukari aina ya pili
Kusafisha ini
Manjano inaweza kusafisha na kutoa sumu zilizoko kwenye damu kwa kupitia vimeng’enyo vyake sambamba na kuongeza uzalishaji wa vimeng’enyo hivyo, hufanya kazi ya kondoa na kunyausha kiwango cha sumu za mwilini.
Husaidia uyeyusho wa chakula tumboni, kuyeyusha mafuta kwenye mishipa ya damu na kusaidia mfumo wa kupandisha kinga, kama kukukinga na mafua, kichefuchefu magonjwa mengine ambukizi.