KAMPUNI ya utengenezaji mabasi yanayotumia nishati jadidifu ya gesiya ETEFA kutoka Austria, imeonyesha nia ya kuwekeza katika mabasi yamwendokasi kwa kuleta mabasi yanayotumia gesi badala ya mafuta.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika kikao na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART,Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Johann Rieger, amesema kampuni yake ina uzoefu wa kutosha wakutengeneza mabasi ambayo hayatumii mafuta, jambo ambalo ni rafiki wa mazingira na pia linasaidiakupunguza gharama za uendeshji
“Mabasi tunayotengeneza yanatumia gesi na nimeelezwa Tanzania mnayo gesi ya kutosha,hiyo ni fursa kwenu kutumia rasilimali kwa ajili ya kuendesha mabasi yaendayo kasi kwani kutumia gesi kunapunguza gharama za uendeshaji kutokana na matumizi ya mafuta kuwa ghari” amesema Rieger.
Amesema endapo watapata fursa ya kuwekeza katika mradi wa mabasi yaendayo kasi ,DART itakuwa mdau wa kwanza nchini kutumia huduma hiyo na itakuwa fursa kwa nchi zingine kuja kujifunza.
Aidha Mtendaji Mkuu amesema kuwa Tanzania kijiografia imekaa eneo zuri katika nchi za Afrika mashariki na kati hivyo ikianzisha kitu chochote ni rahisi kuenea na kwa urahisi na kwa haraka katika nchi zingine zinazoizunguka.
Kutokana na hali hiyo ,amesema kama itaanza kutumia gesi asilia kwenye mabasi ,itapata faida kubwa kwa kuwa itauza gesi na ajira zitaongezeka.