Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu wa Mahakama ya rufaa, Harold Nsekela amefariki dunia leo Jumapili, Desemba 6, 2020 jijini Dodoma baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Marehemu Jaji Nsekela aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na mwezi Februari mwaka 2003 marehemu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, nafasi aliyoitumikia mpaka alipostaafu kwa mujibu wa Sheria.

Marehemu Jaji Harold Nsekela aliteuliwa kuwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mwezi Desemba, 2016, wadhifa aliokuwa nao mpaka alipofariki leo asubuhi.

Rais Dk. John Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia, watumishi wote wa Sekretarieti ya Maadili na Mahakama.

“Jaji mstaafu Nsekela alikuwa mwadilifu , mzalendo, asiyejikweza na mchapa kazi. Mungu amweke mahali pema Amina,” amesema  Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mabasi yanayotumia gesi mbioni kuja nchini
EU na Uingereza ngoma bado nzito

Comments

comments