Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA Ester Bulaya, amehoji suala la miundombinu ya barabara kutokamilika imekuwa ni taatizo sugu na kuhoji ni linio barabara ya Kisorya iliyoko Bunda itakamilika na kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo.
Bulaya ameuliza hayo katika Kikao cha Kwanza cha mkutano wa pili wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amabpo swali hilo lilikwenda katika Wizara ya Ujenzi, huku akieleza kuwa mchakato wa ujenzi wa barabara umechukua takribani miaka 15 sasa.
“Uchelewashwaji wa ukamilishwaji wa miradi ya barabara limekuwa ni tatizo sugu, hapa ninapozungumza ujenzi wa barabara wa kutoka Kisorya, Bunda, ahadi na uanzaji wake umechukua takribani miaka 15, sasa nataka kujua ni lini hiyo barabara itakamilika kwa sababu ikikamilika inaunganisha na barabara ya Serengeti na imekuwa kilio kikubwa kwa wananchi wa mkoa wa Mara”, amesema Mbunge Ester Bulaya.
Ikumbukwe kuwa Ester Bulaya na wenzake 18, walikwishafukuzwa uanachama na chama chao cha CHADEMA, baada ya wao kwenda kula kiapo cha ubunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama chao, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni wasaliti.