Mahakama ya Juu Nchini Kenya imesema kuwa mageuzi ya Kikatiba yanayopigiwa chapuo na Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi Mkuu wa upinzani, Raila Odinga, ni kinyume na sheria za Kenya.
Katika uamuzi wake, Mahakama imesema kuwa Rasimu ya Sheria ya mabadiliko ya kikatiba maarufu kama Building Bridge Initiatives (BBI), ni hatua binafsi ya Rais Kenyatta ambaye hana Mamlaka ya Kisheria kuanzisha mchakato wa mabadiliko yoyote ya Katiba.
Hata hivyo Mpango huo ambao umeligawa Taifa kisiasa, unapendekeza mgawanyo wa Madaraka baada ya Uchaguzi ili kuzuia migogoro ya kila baada ya Uchaguzi katika Makabila hasimu nchini humo.
Tayari Bunge lilishayapitisha marekebisho yaliyopendekezwa ambayo yanaashiria mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa Serikali tangu Katiba mpya kupitishwa mwaka 2010.