Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge amewataka wakazi wa mkoa huo kusherehekea kwa amani na utulivu sikuku ya Eid El Fitr huku akiwataka wazazi na walezi kutowapeleka watoto na kuwaacha wenyewe katika maeneo hatari.

Akizungumza na Dar 24 Media Rc Kunenge amaesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama imejipaga vizuri kudumisha amani katika mkoa wa Dar es Salaama katika kipindi hiki cha sikuku kwa maeneo yote.

Naye Sheikh Alhad Musa amesema mewataka waislam wote kuendeleza uaminifu uliokuwepo kwa mwenyezi Mungu katika mwezi wa Ramadhani na kuendeleza yale mema na kuendelea kusaidi wasio jiweza kama walivyokuwa wakifanya katika mfungo wa Ramadhani.

Bofya hapa kutazama zaidi….

Exclusive: Gharama kubwa za matibabu zachangia matumizi holela ya dawa, "inaua kwa haraka sana"
Waziri Mkuu awasihi Waislamu kuhudhuria Baraza la Eid