Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amemsimamisha kazi kwa siku kumi Meneja wa TEHAMA na huduma za biashara wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Lonus Feruzi na Wasaidizi wake Frank Mushi na Idda Njau ili watoe maelezo kufuatia kuwepo kwa tatizo katika huduma ya manunuzi ya LUKU kupitia njia za kielektroniki na kusema endapo maelezo yao hayatojitosheleza wataondolewa kazini.

Kwa muda wa siku tatu, Wateja wa TANESCO wameshindwa kununua umeme wa LUKU kwa njia ya Kielekroniki hivyo kulilazimu Shirika hilo kuwaelekeza Wateja wake kununua umeme kwenye ofisi zake za Mikoa na Wilaya katika maeneo mbalimbali nchini.

Shirika hilo limewataka wateja kuwa wavumilivu kipindi ambacho wataalamu wanashughulikia tatizo katika mfumo wa manunuzi ya Luku baadhi ya watu walia hasara na kulala giza.

Mtandao wa manunuzi ya Luku ulianza kusumbua tangu Jumatatu ambapo licha ya watu kununua umeme hawakuletewa namba maalumu (token) za kuingiza kwenye mita.

Kwa mujibu wa Tanesco kukosekana kwa huduma ya manunuzi ya Luku kwa baadhi ya wateja kumetokana na hitilafu katika mfumo wa manunuzi Jumatatu ya Mei 17, 2021.

Rais Samia abadilisha Wakuu wa Mikoa wawili
Waziri Bashungwa awaita mashabiki kwa Mkapa.