Kwa dunia ya sasa kujichora tatoo ni kama fasheni fulani kwenye jamii, ukienda kuchora tattoo kuna uwezekano mkubwa sana isitoke maisha yako yote hivyo kwa usalama wako ni vizuri ukamuona mtaalamu wa tattoo ambaye ni maarufu na ana sifa kubwa katika shughuli hizo, anaweza kua ana gharama kubwa lakini binafsi itakusaidia.kwa sasa nchi ya marekani inaongoza kwa kua na watu wengi wenye tattoo duniani.

Madhara yatokanayo na uchoraji Tattoo

Kansa ya ngozi; hapo mwanzoni wataalamu walikua wanasema hakuna mahusiano kati ya kansa ya ngozi na na tabia ya kujichora tattoo lakini hivi karibuni tafiti kutoka uingereza zinaonyesha kuna aina fulani za wino ambazo zinaweza kusababisha kansa zikitumika kuchora tattoo.

Makovu; mwili unataambua tattoo kama adui wake hivyo hujaribu kuiondoa kwa njia mbalimbali na kwa kufanya hivyo husababisha makovu ya muda mrefu ambayo yanaweza kuleta magonjwa mengine ya ngozi.

Zanzibar yapokea vifaa vya Corona

Maambukizi ya ukimwi na ugonjwa wa hepatitis; tabia ya kurudia sindano zilezile wakati wa kuchora tattoo kunaweza kusababisha maambukizi ya virusi vya ukimwi na maambukizi ya virusi vinavyoshambulia ini kitaalamu kama hepatitis b. ugonjwa huu wa hepatitis b husababisha kansa ya ini ambayo haitibiki. ni vizuri kua makini ili uone kama sindano inayotumika kwako ni mpya.

Matatizo kipindi cha kufanya kipimo cha MRI; hichi kipimo ni cha mionzi na kirefu chake ni magnetic resonance imaging, hutumika kupima viungo vya mwili ambavyo havionekani kwa macho ndani ya mwili wa binadamu kama x ray inavyofanya.

Hutaruhusiwa kuchangia damu; mara nyingi watu wenye tattoo hawaruhusiwi kuchangia damu kwani wana hatari ya kusambaza ugonjwa kwenda kwa mtu mwingine, kimsingi mtu aliyechora ndani ya muda mfupi ndio haruhusiwi lakini kwasababu wakati mwingine sio rahisi kutofautisha tattoo mpya na ya zamani basi hawa watu huwa hawaruhusiwi kabisa.mchezaji wa kimataifa christian ronaldo hachori tattoo kwa sababu ya hili.

Tattoo huingiliana na matumizi ya dawa fulani; kama wewe unatumia dawa za kuzuia damu isingane mwilini ukichora tattoo inaweza kufanya utoke damu nyingi sana kwani dawa hizo huzuia uwezo wa mwili kukausha damu na kuponyesha vidonda.

Damu kuganda juu ya ngozi[haematoma]; hii husababishwa na kuvuja kwa damu nyingi chini ya ngozi, huonekana sana pembeni ya sehemu ambapo rangi ya tatoo imepita na huchelewesha kupona kwa kidonda.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 24, 2021
Volcano yalipuka DRC, ujiuji wa moto wafika uwanja wa ndege, Serikali yaagiza watu kuondolewa