Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepokea msaada wa vifaa vya haraka vya kupimia COVID 19 aina ya Rapid Test, vyenye thamani ya shilingi Milion 250 za Kitanzania.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud amepokea msaada huo kutoka kwa kampuni ya SD BIOSENSOR ya nchini Korea.

Makabidhiano hayo ya vifaa vyenye uwezo wa kutoa majibu ya COVID 19 ndani ya dakika 15, yamefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

“Awali vipimo vya COVID 19, vilikuwa vikifanyika zaidi kwa wasafiri ama watu wanaoshukiwa kuwa na maambukizi, lakini kwa msaada huu wa vifaa vipya na vyenye uwezo mkubwa, zoezi la upimaji litaweza kupanua wigo zaidi mpaka katika maeneo ya kijamii,” amesema Masoud.

Masoud amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuweka miundombinu mizuri ya kinga, uchunguzi na namna ya matibabu kwa watakaobainika kuambukizwa ugonjwa huo.

Naye Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, jinsia na Watoto Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, amesema kwa sasa Zanzibar hakuna hata mgonjwa mmoja ambae amethibitika kuwa na COVID 19, ila ameitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhari.

Mwakilishi wa kampuni ya SD BIOSENSOR, Bwana Sunjay Padatia, amesema wao wametoa msaada wa vifaa hivyo ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya janga la corona

Rais Samia ateua mabalozi, wamo Hoyce Temu, Togolani Mavura
Zitto ajilipua, amwandikia haya Rais Samia