Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amekabidhiwa taarifa ya Kamati iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ubadhirifu wa fedha pamoja na matumizi mabaya ya Rasilimali Watu zinazoikabili Bodi ya Utalii Tanzania TTB.
Hatua hiyo inakuja kufuatia Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Devotha Mdachi kusimamishwa kazi mwezi April mwaka huu ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.
Kutokana na hali hiyo ilimlazimu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro kuunda Kamati ya kuchunguza tuhuma hizo iliyoongozwa na Mwenyekiti Mtega ambapo wameikabidhi ripoti mara baada ya kukamilika
Wakati huo huo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Ndumbaro amemkabidhi taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Allan Kijazi kwa ajili ya kuifanyia kazi.