Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amewasili  Paris nchini Ufaransa  ambako atahudhuria Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) linalofanyika Paris Ufaransa kuanzia leo Juni 30 – Julai 2, 202. 

Makamu wa Rais anamuwakilisha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa hilo.

Dkt. Mpango amepata maelezo jinsi Ubalozi wa Tanazania unavyotekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi katika eneo lake uwakilishi ambalo ni Ufaransa,  Hispania; Ureno; Algeria na Morocco.  

Hayo yalielezwa na Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Pia Balozi Shelukindo anaiwakilisha Tanzania katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango amempongeza Balozi Shelukindo kwa uwakilishi mzuri katika nchi hizo na kumuhakikishia serikali itaendelea kutatua changamoto zinazojitokeza katika ubalozi huo.

Amuua mpenzi wake akidai kurudishiwa fedha za matunzo
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 30, 2021