Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Henry Mwaibambe amesema kuwa wananmshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka (30) kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake aitwaye Ester John (28) mkazi wa Ibamba Wilaya Bukombe Mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa Habari amesema kuwa mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake juni 13 mwaka huu akiwa na mtu aliyesemekana ni mpenzi wake ambapo kabla ya kifo chake alitekwa nyara.

Aidha amesema kuwa mwanaume huyo ambaye jeshi la polisi halijamtaja kwa majina yake, alianza kuwapigia simu wazazi wa mwanamke huyo akihitaji kulipwa pesa alizokuwa akimuhudumia kwa ahadi ya kumuoa na kwamba mtuhumiwa alibaini kuwa sio mwaminifu.

“Katika mahojiano alikiri kumteka nyara mwanamke huyo akishinikiza kulipwa gharama alizotumia kumtunza kwa ahadi ya kuoana lakini alibaini kwamba sio mwaminifu, aliposhindwa kurudisha pesa yake ndipo alichukua uamuzi wa kumuua na kumzika huko katika kijiji Masota Wilaya ya Bukombe’’ Kamanda Mwaibambe.

Hata hivyo mtuhumiwa aliwaongoza Askari Polisi mpaka eneo alikomzika ambapo hatua za kisheria zilifuatwa ikiwmo kufukua kaburi na kufanya uchunguzi wa utambuzi wa mwili wa marehemu na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea na upelelezi ukikamilia mtuhumiwa aafikishwa katika vyombo vya sheria.

Wapiganaji wa TPLF waonya vikosi vya Serikali
Dkt. Mpango awasili Ufaransa