Tanzania na India zimekubaliana kuweka msisitizo kwenye uwekezaji katika mnyororo wa uongezaji wa thamani wa madini,vitu vya thamani pamoja na mazao mbalimbali ikiwemo korosho ili kuuza bidhaa badala ya kuendelea na utamaduni wa kusafirisha malighafi.
Hayo yamejiri wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, akipokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule wa India hapa nchini Binaya Srikanta Pradhan,
Ameongeza kuwa njia pekee kwa Tanzania kuongeza ajira na kupunguza umasikini ni kuwekeza katika mnyororo wa uongezaji wa thamani katika bidhaa za kilimo pamoja na madini.
Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Misri hapa Nchini Mohamed Gaber Mohamed juu ya uwekezaji katika sekta ya uvuvi hususani uvuvi katika eneo la bahari lenye kina kirefu (deep sea fishing),viwanda vya nyama na sekta ya afya kwa kujenga hopitali kubwa Jijini Dodoma.