Klabu ya Young Africans rasmi leo Jumatano (Agosti 25) imezindua jezi mpya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Shughuli za uzinduzi wa jezi zimefanywa katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Viongozi, Mashabiki na Wanachama wa Young Africans, huku wakishereheshwa na Mwanafamilia mpya Haji Sunday Manara.

Young Africans wamezindua jezi za nyumbani na ugenini kwa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, sanjari na sare zitakazotumika kwa safari za ndani na nje ya nchi.

Uzinduzi wa Jezi hizo mpya ni sehemu ya Shamra Sharmsa za Wiki ya Mwananchi ambayo ilizinduliwa rasmi mwishoni mwa juma lililopita mjini Unguja Visiwani Zanzibar.

Kilele cha Wiki ya Mwananchi kitakuwa siku ya Jumapili (Agosti 29) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kwa tamasha kubwa la burudani ambalo litaambatana na mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki kati ya Young Africans dhidi ya Zanaco ya Zambia.

Waziri Mulamula akutana na kufanya mazungumzo na watanznia waishio Kenya
Wanawake wazuiwa kufanya kazi Afghanistani