Waziri wa fedha na mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa fedha zilizokusanywa kupitia tozo zitatumika kujenge vituo 220 vya afya
Amesema hayo leo Jumatano Septemba 1, Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari.
Nchemba amesema kuwa wakati Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan anapokea kijiti cha urais jumla ya tarafa 217 zilikuwa hazina vituo vya Afya, lakini makusanyo yote mpaka siku ya jana yatatumika kujenga vituo vya afya na madarasa kwenye tarafa zote ndani ya mwezi mmoja na nusu.
“Vinajengwa vituo 220 tarafa zote na vyenye uwezo wa kufanya upasuaji, wodi za Wanawake na wodi za Watoto, tunakwenda kuokoa maisha ya Wanawake Wajawazito na Watoto.”Amesema Nchemba.
Aidha Nchemba amezitaka taasisi mbalimbali kumuunga mkono Rais kwani Dira aliyonayo ni njema sana na inamatokeo chanya kwenye maendeleo ya Taifa.