Mchambuzi wa Michezo kupitia kituo cha Radio cha EFM Oscar Oscar Jr ameonesha masikitiko yake, baada ya kuona msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara umeanza bila ya kuwa na Mdhamini Mkuu.

Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22 ilianza rasmi Jumatatu (Septamba 27) huku Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ikikaa kimya kuhusu mchakato wa mdhamini mkuu wa Ligi hiyo, baada ya kujitoa kwa Kampuni ya Vodacom mwishoni mwa msimu uliopita.

Oscar ambaye alithubitu kuwania kiti cha Urais wa TFF kabla ya kuenguliwa katika hatua za awali na kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo amesema: “Inasikitisha sana kuona ligi inaanza bila mdhamini mkuu. Hata tuzo za msimu uliopita hazijatolewa, kwangu mimi hata wakisema tuzo zinatolewa saizi zitakuwa hazina maana Tena, kwasababu zilishapoteza maana kutokana na wachezaji na makocha wengine waliokuwepo msimu uliopita walishaachana na Vilabu vyao”

“TFF na Bodi ya ligi inatakiwa ilaumiwe katika hili, sababu hatakama wanasema mdhamini aliyepita alijitoa katikati mwa ligi, tuzo za msimu hazihitaji mdhamini mkuu hata wao wenyewe wangeweza kuiandaa Kama tafrija flani wiki moja kabla au baada ya ligi kuisha”

“Kwa upande mwingine hata vilabu vyetu inatakiwa vitafute wadhamini wao sababu hata Jezi zikijaa makolokolo Wala haina shida. Vilabu ndio vinapaswa vitafute mdhamini na kumuelezea atafaidika vipi iwapo ataidhamini timu yao, na siyo kusubili mdhamini kutafuta klabu”

“Lakini pia naipongeza TFF kwa kusaini mkataba na Azam TV wa TV right, sababu ukiangalia hata EPL, mapato makubwa yanapatikana katika TV right ukilinganisha na mapato kutoka sehemu nyingine.”

Dkt. Ndumbaro atoa maagizo kwa watumishi wa Umma
Mwili wa Ole Nasha kuzikwa jumamosi