Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, kimeondoka jijini Mwanza kuelekea jijini Dodoma kupitia Dar es salaam, tayari kwa mchezo wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu 2021/22.

Simba SC ilikua mkoani Mara katika mji wa Musoma kwa ajili ya mchezo wa mzunguuko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, na kuambulia sare ya 0-0 dhidi ya wenyeji Biashara United Mara, jana Jumanne (Septamba 28).

Mapema hii leo kikosi cha Simba SC kiliondoka mjini Musoma kuelekea Mwanza, kabla ya kuendelea na safari ya Dodoma kupitia Dar es salaam.
Ikiwa Jijini Dodoma Simba SC itacheza mchezo wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC Jumamosi (Oktoba 02), katika Uwanja wa CCM Jamhuri.

Dodoma Jiji FC ilianza viziri Mshike Mshike wa Ligi Kuu 2021/22 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, jana Jumanne (Septemba 28).

Mwili wa Ole Nasha kuzikwa jumamosi
Biashara United walamba Milioni 10