Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Chelsea na Atletico Madrid Diego Costa kwa sasa yupo huru kujiunga na klabu yoyote itakayohitaji huduma yake, baada ya kuondoka Atletico Mineiro ya Brazil.

Costa aliachana na klabu hiyo mwezi uliopita ambako alikuwa akilipwa mshahara wa pauni 46,000 kwa wiki, na sasa anatafuta mahala ambapo ataendelea kuonyesha uwezo wake wa kupachika mabao.

Kwa mujibu wa gazeti la Bild, mshauri wa Mainz alipongeza huduma ya mshambuliaji huyo kwa kutuma ujumbe kwa mmoja wa maskauti wao kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Costa alitaka mkataba wa miezi 18, lakini skauti wake hakuichukulia ofa hiyo kwa uzito mkubwa.

Suala hilo lilifanya taarifa sahihi juu ya uwezekano wa dili hilo kutomfikia Mkurugenzi, Martin Schmidt kwa wakati, kutokana na dau alilotaja Costa.

Zaidi inadaiwa mkurugenzi naye alipoambiwa baadaye akasema hata angekuwa yeye asingeamini uzito wa ofa hiyo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, klabu ingeweza kumlipa takribani euro milioni nne kwa mwaka kama alivyotaka.
Barcelona na Arsenal wanatajwa walikuwa kwenye hatua za kufanya uamuzi juu ya nyota huyu pia.

Rafiki yake John Terry anashindwa kuamini Costa amekosa klabu hadi sasa, lakini inatajwa kwamba, Fenerbahce inamtaka.

Wizara ya ardhi yatoa tahadhari
Rais Samia aagiza kuu dwa kamati nyingine ya uchunguzi